Jumatano 22 Oktoba 2025 - 20:05
Fadhila Saba za kunyamaza

Hawza News/ Imam Ṣādiq (a.s.) katika riwaya yenye maana pana, ameeleza kuwa kukaa kimya si tu njia ya watafiti, bali ni chanzo cha kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kinga dhidi ya makosa.

Shirika la Habari la Hawza - Amīrul-Mu’minīn (a.s.) kuhusiana na umuhimu wa kukaa kimya amesema:

«بِکثْرَةِ الصَّمْتِ تَکونُ الْهَیبَةُ»

“Kwa kukithirisha kunyamaza huzalisha heshima na ukubwa.”

Sherehe:
Kuhusu umuhimu wa kunyamaza, maneno mengi yamesemwa, na hadithi nyingi zimepokewa juu ya jambo hili.
Imepokewa kutoka kwa Imam Sa'diq (a.s.) riwaya ambayo ndani yake zimetajwa fadhila nyingi za kunyamaza, amesema:


Kunyamaza ni njia ya watafiti wa kweli, na ni kanuni ya wale wanaotafakari hali za waliopita na kuelewa mabadiliko ya zama; kwa yakini, tafakuri hiyo ndiyo msingi wa kunyamaza na utulivu.

Radhi za Mwenyezi Mungu zimo ndani ya kunyamaza , nalo ni sababu ya kuifanya hesabu iwe nyepesi na kinga dhidi ya makosa na upotovu.

Mwenyezi Mungu amekufanya kunyamaza kuwa ni pazia la kuficha ujinga na pambo kwa wenye elimu.

Kunyamaza ni njia ya kujiepusha na matamanio, ni mazoezi ya nafsi, ni utamu wa ibada na ni tiba ya ugumu wa moyo.

Kunyamaza husababisha kuchunga, ushujaa na werevu.

Basi zuia ulimi wako usifunguke kwa maneno yasiyo ya lazina kuyasema, hasa pale usipompata msikilizaji mwema ambaye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika njia ya Mwenyezi Mungu unazungumza naye. (2)

Imeelezwa kuwa mmoja wa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiweka kokoto ndani ya kinywa chake, na kila alipokusudia kusema, aliitafakari; ikiwa angeona kuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika njia ya Mwenyezi Mungu, ndipo angeitoa mdomoni. (3)

Kwa hivyo, ili tuwe salama dhidi ya makosa, dhambi na upotovu mwingi unaotokana na kuzungumza kupita kiasi, tunapaswa kupambika kwa nguvu ya “kunyamaza.”
“Na taufiki ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” 

Rejea:
1. Nahjul-Balāgha, hekima ya 224

٢- «اَلصَّمْتُ شِعَارُ اَلْمُحَقِّقِینَ بِحَقَائِقِ مَا سَبَقَ وَ جَفَّ اَلْقَلَمُ بِهِ وَ هُوَ مِفْتَاحُ کُلِّ رَاحَةٍ مِنَ اَلدُّنْیَا وَ اَلْآخِرَةِ وَ فِیهِ رِضَی اَللَّهِ وَ تَخْفِیفُ اَلْحِسَابِ وَ اَلصَّوْنُ مِنَ اَلْخَطَایَا وَ اَلزَّلَلِ وَ قَدْ جَعَلَهُ اَللَّهُ سِتْراً عَلَی اَلْجَاهِلِ وَ زَیْناً لِلْعَالِمِ وَ مَعَهُ عَزْلُ اَلْهَوَی وَ رِیَاضَةُ اَلنَّفْسِ وَ حَلاَوَةُ اَلْعِبَادَةِ وَ زَوَالُ قَسْوَةِ اَلْقَلْبِ وَ اَلْعَفَافُ وَ اَلْمُرُوَّةُ وَ اَلظَّرْفُ فَأَغْلِقْ بَابَ لِسَانِکَ عَمَّا لَکَ مِنْهُ بُدٌّ لاَ سِیَّمَا إِذَا لَمْ تَجِدْ أَهْلاً لِلْکَلاَمِ وَ اَلْمُسَاعِدَ فی اَلْمُذَاکَرَةِ لِلَّهِ وَ فِی اَللَّهِ.»
مصباح الشريعة، ج١، ص ١٠١.

٣- «وَ کَانَ بَعْضُ أَصْحَابِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّی اَللَّهُ عَلَیْهِ وَ آلِهِ یَضَعُ اَلْحَصَاةَ فِی فَمِهِ فَإِذَا أَرَادَ أَنْ یَتَکَلَّمَ بِمَا عَلِمَ أَنَّهُ لِلَّهِ وَ فِی اَللَّهِ وَ لِوَجْهِ اَللَّهِ أَخْرَجَهَا مِنْ فَمِهِ.»
مصباح الشريعة، ج١، ص ١٠١.

Imeandaliwa na Idara ya Elimu na Utamaduni ya Shirika la Habari la Hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha